Wednesday, July 9, 2014

RAIS Obama aomba msaada wa dharura


Rais Barack Obama

RAIS  Obama anaomba dola bilioni 3.7 za msaada wa dharura kutoka bunge la Marekani kusaidia kukabiliana na ongezeko la watoto waliohama peke yao kutoka Amerika ya kati.

Ikulu ya Marekani inasema fedha hizo zitasaidia kupunguza kile maafisa wanakitaja kuwa hali ya dharura ya kibinaadamu iliyoshuhudia watoto zaidi ya elfu hamsini na mbili waliohama peke yao kutoka El Salvador, Guatemala na Honduras kuvuka kiharamu mpaka wa Marekani tangu mwezi Oktoba mwaka jana
Umaskini na ongezeko la hivi karibuni la ghasia zinazohusiana na magenge na mitandao ya ulanguzi madawa ya kulevya zimesababisha ongezeko la wahamiaji kutoka eneo hilo la Amerika ya kati.

Wengi wao watoto ambao wameingia Marekani kupitia bonde la Rio Grande huko Texas.












No comments:

Post a Comment