![]() |
| Waziri wa Habari wa Somalia Mustafa Dhuhulow |
VIKOSI vya
serikali Somalia vimefanikiwa kuidhibiti upya Ikulu ya rais katika mji mkuu
Mogadishu baada ya wapiganaji wa Al Shabaab kuishambulia.
Maafisa wanasema washambuliaji
wapatao watano kutoka kundi la al-Shabab - waliuawa walipoingia katika eneo la
ikulu hiyo.
Washambuliaji hao wanadaiwa kulipua
bomu lililotegwa kwenye gari karibu na langu kuu la Ikulu hiyo.
Waziri wa habari na mawasiliano wa Somalia
Mustaf Dhuhulow ameviambia vyombo vya habari kuwa tayari mmoja wa washambuliaji
hao amekamatwa na anahojiwa na polisi.
No comments:
Post a Comment