MWENYEJI
wa michuano ya soka ya Kombe la Dunia la mpira
wa miguu, Brazil ametolewa na Ujerumani katika mechi ya nusu fainali
iliyofanyika jana baada ya kufungwa mabao 7 kwa 1 katika uwanja wa Mineirao.
Ujerumani ilianza kuongoza kwa bao la
kwanza lililofungwa na Thomas Muller katika dakika ya 11 baada ya kupigiwa
mpira wa kona kutoka upande wa kulia.
Goli la Muller lilifuatiwa na goli la
pili lililofungwa na mchezaji mwenzake Miroslav Klose katika dakika ya 23.
Akizungumzia mechi hiyo kocha wa Ujerumani Joachim Loew amesema kuwa, mwenyeji
Brazil alishindwa kukabiliana na mashambulizi ya kila upande ya Ujerumani.
Sasa timu ya Taifa ya Ujerumani
itakutana Jumapili ijayo katika fainali ya kombe la dunia na mshindi wa nusu
fainali kati ya Argentina na Uholanzi.

No comments:
Post a Comment