MWENYEKITI wa halmashauri ya wilaya ya Kilosa Ameir Mubaraka Nahdi amewaagiza
viongozi wa vijiji vya kata Lumuma wilayani humo kutumia
kipindi hiki cha kiangazi kuwaondoa wafugaji wote wavamizi wa maeneo ya
wakulima.
Agizo hilo alilitoa
kitongojini Manyomvi katika sherehe ya mkulima iliyoandaliwa na mradi wa
mpango wa kupunguza hewa ukaa inayotokana na uharibifu na ufyekaji ovyo wa
misitu MKUHUMI chini ya shirika la kuifadhi misitu ya asili Tanzania TFCG.
Kwa mujibu wa Mubaruk serikali
wilayani humo imechoshwa na kelele baina ya wakulima na wafugaji ambazo kwa
muda mrefu zimeiweka wilaya hiyo kwenye ramani ya machafuko ya migogoro ya
ardhi kwa muda mrefu.
Awali afisa kilimo wa mradi wa
mkuhumi Shadrack Nyungwa alieleza lengo la maadhimisho ya sherehe hiyo ni
kupongezana na kupeana zawadi na kuhamasisha jamii kuongeza bidii ya utunzaji
mazingira shambani.
Vijiji 8 vimeshiriki na
kupatiwa mafunzo ya kilimo hifadhi na mazingira ambavyo ni
Manyomvi,mlenga,Idete na Mfuluni, vingine ni Kisongwe, Lunenzi, Ibingu
na chabima.

No comments:
Post a Comment