![]() |
| Wanawake wa Mazimbu Morogoro |
WATANZANIA wameshauriwa
kuliangalia kundi la watoto wanaozaliwa kwenye mazingira hatarishi,wakiwa na
upungufu wa akili badala ya kuwanyanyapaa na kuwatelekeza kama inavyojitokeza
katika maeneo mbalimbali nchini.
Baadhi ya wanawake wa Mkoani
Morogoro walisema hayo wakati wakizungumza walipotembelea kituo cha kulelea
watoto wanaoishi katika mazingira magumu na walio na upungufu wa akili cha
Mehayo, kilichopo Mazimbu Mkoani Morogoro.
Mmoja wa wanawake hao, Elizabeth
Mtambo, ambaye pia ni makamu Mwenyekiti wa Kikundi cha wanawake cha Kizota,
kutoka chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA, alisema tabia ya baadhi ya wazazi
na walezi kuwatelekeza watoto wenye matatizo ya akili na waishio katika
mazingira magumu,imesababishwa na ukosefu wa elimu ya kutosha kuhusu umuhimu wa
watoto hao, na kulaani baadhi ya wanawake wanaoshiriki ukatili huo.
Aidha Mlezi wa kituo cha Mehayo,
Prisca Chinyama, aliishauri Serikali katika kukabiliana na hali hiyo, ni vyema
wakaangalia uwezekano wa kutunga sheria kali ili kuwabana watakaobainika
kuwanyanyasa watoto wenye matatizo ya akili na walio katika mazingira magumu.

No comments:
Post a Comment