![]() |
| RAIS Rouhan akihutubia katika maonesho ya kimataifa ya Qur'an |
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema matatizo wanayokumbana nayo Waislamu hivi sasa ni matokeo ya kutoyazingatia mafundisho ya Qur'ani Tukufu.
Rais Rouhani aliyasema hayo Jumamosi usiku alipohutubu katika Maonyesho ya 22 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu mjini Tehran.
Akihutubu katika mahafali maalumu iliyofanyika kwa lengo la kuwaenzi wanaoihudumia Qur'ani, Rais Rouhani ameashiria sifa za kipekee za Qur'ani Tukufu.
Amesema pamoja na kuwepo mitazamo tafauti katika kufahamu na kuifasiri Qur'ani Tukufu, lakini kwa bahati nzuri hakuna hitilafu kuhusu aya na yaliyomo katika Qur'ani Tukufu na hivyo kitabu hicho kitukufu ndicho chanzo kikuu cha Umoja wa Kiislamu. Rais wa Iran amesema Waislamu wanapojikurubisha kwa Qur'ani Tukufu huweza kufahamu maana ya aya za kitabu hicho kitakatifu na hivyo kutekeleza maamurisho yake maishani.

Waislamu wengi wana ushabiki wa dini.Kwani madhehebu asili yake ?
ReplyDeleteTUSAIDIANE NAMANA YA KUWAELIMISHA WAISLAMU WA ULIMWENGU HASA MASHARIKI YA KATI
ReplyDelete