WAZIRI wa Habari wa
Liberia Lewis Brown ameiambia waandishi kwamba mfumo wa afya wa nchi hiyo
umeyumbishwa na athari zilizotokana na mlipuko huo wa ugonjwa wa Ebola.
Kikosi cha jeshi nchini humo kimetawanywa kuweza kuwazuia watu wasisafiri
kuingia katika mji mkuu wa nchi hiyo, kutoka katika maeneo ya vijiji
yaliyokumbwa na ugonjwa huo.Wakati huohuo katika nchi jirani ya Sierra Leone, ambayo maeneo yote yamewekwa vizuizi kujaribu kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo. Waziri wa Habari wa nchi hiyo Alpha Kanu amesema inakatisha tamaa kuona kwamba dawa ambazo bado ziko katika majaribio, hazijasambwazwa nchini himo
No comments:
Post a Comment