![]() |
| Waziri wa Afya na ustawi wa jami Dk Seif Rashidi |
BAADHI ya wananchi
jijini Dar es salaam wameipongeza wizara ya Afya na ustawi wa jamii kwa hatua
yake ya kuzuia uuzwaji wa dawa za binadamu katika nyumba za ibada.
Wakionhea na waandishi
wa habari jijini Dar es salaama mapema leo, baadhi ya wanunuzi wa dawa
zinazouzwa katika misikiti mbalimbali jijini Dar wamesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya watu
kujitambulisha kama madakatari bingwa wa baadhia ya magonjwa ilihali hawana
hata elimu ya ngazi ya cheti juu ya mambo ya utabibu.
Hata hivyo wameitaka
wizara husika kutoishia kwa wauzaji dawa wa misikiti bali iende mbali zaidi hata kwa waganga wa jadi
ambao nao wanafanyabiashara katika maeneo mbalimbali hapa nchini , baadhi yao
hawana taaluma ya utabibu wala udaktari.

No comments:
Post a Comment