![]() |
| Waujmbe wabunge la katiba |
HABARI kutoka Dodoma Tanzania katika vikao
vya Bunge maalumu la Katiba zinasema kuwa, majadiliano ya bunge hilo yamefungwa
baada ya muda wa kufanya hivyo kumalizika.
Taarifa
zaidi zinasema kuwa, keshokutwa Alkhamisi ndiyo siku ambayo rasimu ya mwisho
inayopendekezwa na Bunge Maalumu la Katiba, itatolewa hadharani mbele ya Bunge
hilo na Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi, Andrew Chenge.
Jana kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta, ndio ilikuwa siku ya mwisho
ya majadiliano.
Leo Jumanne
na kesho Jumatano, hakutakuwa na vikao vya Bunge, badala yake wajumbe wote
watakutana kwenye semina mbalimbali, ikiwemo iliyoandaliwa na Bunge hilo wakati
wanasubiri Katiba mpya kuwasilishwa bungeni.

No comments:
Post a Comment