Tuesday, September 16, 2014

VIONGOZI WA siasa na kijamii watakiwa kuwa makini kuelekea uchaguzi mkuu



Mwenyekiti wa kituo cha Demokrasia nchini John Cheyo

TAHADHARI ya utumishi wa haki na sheria imetolewa kwa viongozi wa serikali na vyama vya Siasa nchini wakitakiwa kuwa makini kwa kufuata sheria,kanuni na taratibu za uongozi kwenye utumishi wao ili kuliepusha taifa na machafuko ya kisiasa wakati huu wa kuelekea kwenye chaguzi za uongozi wa serikali za mitaa na serikali kuu.


Thadhari hiyo imetolewa na mtafiti na mshauri wa mambo ya kisiasa na utawala bora kutoka taasisi ya ‘diligent international colsult Ltd’(DICL) Godlisten Moshi kwenye mafunzo ya utawala bora na ufutiliaji rasilimali za umma kwa madiwani,maafisa watendaji na maofisa kutoka halmashari ya wilya ya Morogoro yaliyoandaliwa na mtandao wa jinsia nchini TGNP.

Moshi alisema kuepusha hilo linaloweza kuepusha kugharimu maisha ya watanzania wengi kutokana na malezi waliyoanayo, kila kiongozi anapaswa kufuata sheria,kanuni na taratibu za utumishi wakiepuka viashiria vya machafuko ikiwemo rushwa na upendeleo au maagizo yaliyo kinyume na utawala bora..

Baadhi ya washiriki wa amfunzo hayo akiwemo Diawani wa kata ya Mkambarani Daniel Shawa na Afisa mtendaji kata hiyo Camilious Lyimo mbali na kukili kuwepo kwa dalili hizo walisema pia vishawishi hivyo vinatokana na changamoto ya ugumu wa maisha na kutojali hususani katika masula yenye manufaa kwa maisha yao.

No comments:

Post a Comment