WANAJESHI kumi na wawili nchini Nigeria wamepewa adhabu
ya kifo kwa uasi pamoja na jaribio la mauaji.
Hii ni baada ya kumfyatuliwa bunduki
afisa mkuu anayeongoza operesheni ya kupambana dhidi ya kundi haramu la
kiislamu la Boko Haram kati mji wa Maiduguri,kaskazini Mashariki mwa nchi,
mwezi wa Mei.
Wanajeshi wengine watano
waliachiliwa baada ya ushahidi kukosekana.
Wanajeshi hao 12 walipatikana na
hatia ya kumfyatulia risasi Jemedari amadu Mohammed.
Wanajeshi hao walikasirishwa na
kamanda wao ambaye walimlaumu kwa kukataa kuchukua hatua baada ya msafara wao
kushambuliwa.
Jeshi la Nigeria limeshindwa
kuwashinda Boko Haram na wanajeshi wamekuwa wakilalamika kuwa kila
wanapokabiliana na wapiganaji wa Boko Haram hawana silaha za kutosha
kukabiliana nao.
Wote walikana mashtaka hayo katika
Mahakama ya kijeshi mjini Abuja.
Kitengo hicho cha Jeshi ndicho
kinakabiliana na Boko Haram
Mahakama ya kijeshi ya watu tisa
ilisikiza kuwa tukio hilo lilitendeka baada ya kufyatuliwa kwa risasi kwa afisa
mkuu wa kitengocha 7 cha jeshi la Nigeria.

No comments:
Post a Comment