Tuesday, September 16, 2014

POLISI sita wauwawa nchini Misri



ASKARI  polisi 6 wameuawa katika mlipuko katika rasi ya Sinai Misri wizara ya maswala ya ndani ya Misri imetangaza.

Polisi hao waliuawa bomu lililokuwa limetegwa kando ya barabara ilipolipuka msafara wa polisi ukipita.
Maafisa wawili zaidi walijeruhiwa vibaya katika tukio hilo.
Wanamgambo katika rasi ya Sinai wameendeleza mashambulizi zaidi haswa baada ya kung'olewa mamlakani kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Mohammed Morsi mwaka uliopita.


No comments:

Post a Comment