![]() |
| Ofisi za posta nchini Israel |
WAFANYAKAZI wa Idara ya Posta ya Israel wamegoma wakilalamikia mpango wa kufukuzwa wafanyakazi wenzao 1500.
Utawala wa Kizayuni wa Israel unapanga kuwafukuza wafanyakazi 1500 wa idara ya posta na badala yake iwaajiri kwa muda na kwa mkataba wafanyakazi wengine.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, huduma katika posta huko Israel zimesimama kutokana na wafanyakazi wa idara hiyo kugoma kufanya kazi wakilalamikia uamuzi huo. Katika miezi iliyopita Waisraeli wengi wamehajiri na kukimbilia Ujerumani na Marekani kwa matumaini ya kupata kazi kutokana na hali mbaya ya kiuchumi inayotawala huko Israel. Katika miaka ya hivi karibuni maisha ya Waisrael hasa wa tabaka la kati yamekuwa magumu kutokana na kodi kubwa na mishahara midogo. Waisrael wamekuwa wakiandamana katika mji wa Tel Aviv na miji mingine ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu wakilalamikia mpango wa kiuchumi pamoja na siasa za kubana matumizi za viongozi wa utawala huo ghasibu. Siasa za kubana matumizi

No comments:
Post a Comment