Tuesday, September 16, 2014

MAREKANI bingwa wa kikapu kombe la dunia


Waserbia wakimdhibiti mchezaji wa Marekani

MAREKANI  imetawazwa Mabingwa wa kombe la Dunia wa mchezo wa mpira wa kikapu kwa kuichapa Serbia vikapu 129 kwa 92. Marekani wameutetea ubingwa wao waliouchukua huko uturuki mwaka 2010.

Angola na Senegal ziliiwakilisha afrika ingawa hazikufika mbali sana.
Kombe la Dunia la Mpira wa Kikapu la Mwaka huu wa 2014 lilikuwa toleo la 17 la FIBA Basketball World Cup kwa kuwa hapo awali michuano hi ilifahamika kama FIBA World Championship.
Michuaono hii iliyofanyika Hispania ni ya mwishopkufanyika katika mzunguko wa miaka mnne kwani michuano ijayo itafanyika miaka mitano ijayo yaani mwaka 2019 ili kurekebisha hesabu za miaka kuingilia ratiba ya Kombe la Dunia na Fifa.
Katika ligi kuu ya England, ushindi wa Manchester United wa mabao 4-0 dhidi ya Queens Park Rangers umempa nguvu meneja wa timu hiyo Luis Van Gaal na kusema kuwa matarajio yake ni kurejesha taji la ligi katika uwanja wao.





No comments:

Post a Comment