MAZISHI ya mvulana
mdogo mpalestina, ambaye aliuwawa katika kisa cha kutekekezwa moto nyumba kwao
huko West Bank, yamefanyika.
Mtoto huyo wa miezi 18 alifariki
baada ya nyumba yao iliyoko katika kijiji cha Duma kusini mwa mji wa Nablus,
kuteketezwa kwa moto baada ya kumwagiwa petroli.
Wazazi wa mtoto huyo na kaka yake
pia walijeruhiwa katika shambulizi hilo.
Waziri mkuu wa Israeli, Benjamin
Netanyahu ameyataja kama lilikua tendo la ugaidi.
Wakazi wa kijiji hicho wanasema
waliofanya shambulizi hilo waliandika neno "kisasi" kwa kiyahudi
kwenye ukuta na kuweka nyota ya Mfalme Daudi.
Mwaandishi wa kidiplomasia wa BBC
mashariki ya kati anasema kuwa, shambulio hilo linafanyika wakati ambapo hali
ya usalama ni tete kati ya Israeli na Palestina, huku hali ya taharuki ikitanda
kati ya kundi moja la walowezi la wa mrengo wa kulia na serikali ya Israeli.
Serikali ya Israeili imetaja mauaji
hayo kuwa ya ''kigaidi''.
No comments:
Post a Comment