SHIRIKA la ndege la taifa (ATCL) limerejesha safari zake kuelekea mkoani
Mwanza ikiwa ni sehemu ya mpango wa shirika hilo kupanua huduma kwa wateja wake
hapa nchini.
Safari ya kwanza ya shirika hilo kuelekea mkoani Mwanza ilifanyika mwishoni mwa
juma lilopita kwa kukutumia ndege yake aina ya CRJ- 200, baada ya safari hizo
kusimama tangu mwezi Agosti mwaka mwaka jana.
Akizungumza na waandishi wa habari
mara tu baada ya kuwasili kwa ndege hiyo Uwanja wa ndege wa Mwanza, Kaimu Afisa
Uhusiano wa Shirika hilo, Bi Lily Fungamtama alisema uamuzi wa kurejesha safari
hizo umezingatia mahitaji ya wateja wa shirika hilo.
“Tumepokea maombi mengi kutoka kwa
wateja wetu wakiwemo wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao kwa kuhusisha
majiji haya mawili. Kwa kuwa ATCL ni shirika mama la ndege hapa nchini
tukafanya kila jitihada kuhakikisha tunarejesha safari zetu kuelekea jijini
Mwanza,’’
alibainisha Fungamtama huku
akiongeza kuwa shirika hilo litafanya safari zake mara mbili kwa siku katika
siku zote saba za wiki.
Alisema ili kukabiliana na ushindani wa kibiashara dhidi ya mashirika mengine ya ndege yanayofanya safari zake kuelekea mkoani humo, shirika hilo limewekeza zaidi kwenye ubora wa huduma zake sambamba na kutoa huduma zake kwa gharama nafuu.

No comments:
Post a Comment