Thursday, August 20, 2015

MKUU wa jeshi la magereza nchini , kamishina John Minja aombwa kutembelea gereza la Mbigili ,wilayani Kilosa



ASKARI  Magereza wa Gereza la Mbigili Wilayani Kilosa wakimwomba mkuu wa jeshi hilo nchini, Kamishina John Minja kuwatembelea ghafla na kuzungumza nao katika gereza hilo ili wamweleze bayana ufujwaji fedha na rasilimali za umma unaofanywa na mkuu wa gereza hilo.


Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa sharti la kutotajwa majina yao,baadhi ya asikari katika gereza hilo wakimtaja mkuu huyo SSP.Charles Kimbi walisema tangu aingie kuongoza gereza hilo Mwaka jana amekuwa akifuja mali za umma kwa manufaa yake sambamba na kuwanyanyasa asikari hao kinyume na taratibu za utumishi ndani ya jeshi hilo. 

Hata hivyo alipotafutwa kutoa ufafanuzi wa madai yanyomkabili mbali na kushindwa kukili au kukataa, alimtaka mwandishi wa habari hizi kumtajia waliomfikishia taarifa hizo na kumtaka maswali hayo kuwasiliana na Kamishina Minja au mkuu wa magereza mkoa RPO Kato Ruginnura.

Baadhi ya mambo ambayo amekuwa akiyafanya kwa manufaa take kwa muijibu wasikari hao ni pamoja na Kukodisha ardhi ya serikali kwa shilingi 50,000 kwa ekari Mpunga na Mahindi huku akipiga marufuku kwa mtumishi kulima katika eneo hilo zaidi ya eka moja.

Kwa mujibu wa asikari hao mkuu huyo wa gereza SSP Kimbi amejimilikisha mradi wa klabu'Bwalo' ulioanzishwa na asikari hao kwa ajili ya kusogeza huduma ya vinywaji na burudani mbalimbali huku akiwalazimisha kuendelea kuchangia gharama za uendeshaji ikiwemo Umeme na kulipia king'amuzi cha DSTV.

Aidha walisema Kigogo huyo amefuta utaratibu wa asikari kupewa siku sita nje ya siku 28 za sheria kwa ajili ya mamatizo ya njiani aendapo likizo na kurudi sambamba na kupiga marufuku watumishi hao kufyatua tofari za kuchoma kwa ajili ya kujiandalia makazi baada ya kustaafu.


Katika ufafanuzi wake Mkuu wa magereza Mkoa RPO Kato Ruginnura mbali na kushindwa kutoa ufafanuzi wa taasisi hiyo kuruhusu ukodishwaji maeneo yake na fedha zinazokusanywa kwa wakodishwaji na walishaji mifugo kutofahamika ziendako alikili jeshi kutoa siku sita kwa upendeleo hasa kwa asikari wa mikoa ya mbali na kituo.
Alisema kuhusu Mabwalo yaliyo kwenye magereza nchin kote ni sehemu ya utawala kwakua lengo ni kumwezesha asikari  kambini na familia zao kuwa na sehemu ya kupumzika hasa baada ya kazi za siku.


No comments:

Post a Comment