Saturday, August 1, 2015

MAMIA nchini Mali wafurika kujionea muujiza wa kidini


wananchi nchini Mali wakishangaa katika eneo la tukio

MAELFU ya raia katika mji mkuu wa Mali Bamako wanaendelea kufurika ili kujionea kile kilichotajwa kuwa muujiza wa kidini katika ukuta mmoja ambao ulionekana wikiendi iliopita.

Wengi wanaamini picha hiyo nyeupe katika ukuta wa nje wa choo inamuonyesha mtu akisali na kuonekana kama ishara ya ujumbe wa Mungu.
Maafisa wa polisi wa kukabiliana na ghasia walipelekwa katika eneo hilo ili kudhibiti umati huo kwa kuwa watu wanapiga foleni usiku kucha kuona muujiza huo wa alama.

No comments:

Post a Comment