TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Arusha, imewaburuza mahakamani vigogo watatu wa Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia (Camartec), kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi.
Ilidaiwa mbele ya Hakimu Patricia Kisinda wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Arusha/Arumeru kuwa, watuhumiwa hao walitoa zabuni ya matengenezo ya gari kwa kampuni ya Mbilinyi Auto Garage ambayo malipo yake yalikuwa Sh. 24,820, 000.
Mawakili wa Takukuru, Monica Kijazi na Rehema Mteta, walidai kuwa utaratibu wa kutoa zabuni ya matengenezo ya gari hiyo aina ya Toyota Land Cruizer ulikiuka Sheria ya Manunuzi na matumizi mabaya ya ofisi kinyume cha Sheria ya Takukuru.
Vigogo walioburuzwa mahakamani hapo ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Camartec, Elifariji Makongoro, Ofisa Manunuzi Absalom Nnko na Kaimu Ofisa Usafiri, Pythias Ntella.
Walidaiwa kwa kukiuka sheria hizo waliisababishia hasara Camartec ya Sh. 24, 820,000.
Hata hivyo, watuhumiwa hao wote walikana kutenda makosa hayo.
Mahakama ilisema kosa wanalotuhumiwa watuhumiwa hao lina dhamana na hakimu ali
No comments:
Post a Comment