Saturday, November 28, 2015

PAPA Francis awasili nchini Uganda

Papa Francis akiwasili nchini Uganda 
KIONGOZI wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis amewasili nchini Uganda kwenye sehemu ya pili ya ziara yake Afrika.

Papa amelakiwa katika uwanja wa ndege wa Entebbe na Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
Baadaye, Papa anatarajiwa kuelekea ikulu ya Rais mjini Entebbe, kisha ahutubie maafisa wa serikali na mabalozi humo ikuluni.
Baadaye atawahutubia walimu.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir pia yumo nchini Uganda kukutana na Papa Francis.


No comments:

Post a Comment