![]() |
| Mkuu wa mkoa wa Morogoror Dk Rajabu Rutengwe |
SERIKALI mkoani Morogoro imepiga marufuku biashara
holela za matunda,mbogambaoga,juisi na aina zote za vyakula katika
maeneo ya mikusanyiko ya watu zikiwemo stendi za mabasi kuunga mkono agizo la
Rais Dk.John Magofuli kuweka miji safi na kutokomeza maambukizi ya ugonjwa wa
Kipindupindu.
Agizo hilo limetolewa na
Mkuu wa mkoa Morogoro Dk.Rajabu Rutengwe wakati akizungumza na waandishi wa
habari ofisini kwake juu ya azima ya mkoa kuunga mkono tamko la Rais kufuta
maadhimisho ya siku ya uhuru 9 Desemba badala yake kufanya usafi katika miji nchini.
“mwaka huu inatimia
miaka 54 ya Uhuru wa Taifa letu, jukumu letu ni kutekeleza agizo la Rais
Dk.Magufuli na mpango kazi wetu ni kufanya usafi kuondoa maambukizi ya Kipindu
pindu kilichoripotiwa kwa mara ya kwanza tarehe 18/8/2015 Manispaa ya Morogoro
baadae wilayani Gairo,Kilombero,Mvomero na Ulanga”alisema Dk.Rutengwe.

No comments:
Post a Comment