CHAMA cha
mapinduzi CCM wilayani Kilombero kimempongeza Rais wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania Dk.John Magufuli kwa kasi aliyoanza nayo na kuahidi kumuunga mkono kwa
juhudi hizo.
Aidha alimpongeza Rais Dk.Magufuli kwa umakini wake uliomwezesha
kumpata na kumteua Majaliwa Kasimu Majaliwa kuwa waziri mkuu wa serikali ya
awamu ya tano nchini.
Hayo yalisemwa na wenyekiti wa ccm wilayani humo Abdallah
Kambangwa wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake na kuahidi
kumuunga mkono wakati wote awapo madarakani.
Katika mazungumzo hayo Kambangwa alisema hotuba ya ufunguzi wa
Bunge mjini Dodoma iliakisi maneno na ahadia alizokuwa akizisema wakati wa
kampeni na kuongezwa nguvu na utekelezwaji ahadi hizo anaoufanya sasa.
Amewataka watanzania kumuunga mkono kwa uteuzi wake na kumpa
ushirikiano yeye pamoja na wateule wake katika kutekeleza kauli mbiu ya
serikali ya awamu ya tano ya hapa kazi tu.
Akielezea malengo yao baada ya uchaguzi ambapo chama hicho
kimepoteza majimbo mawili ya Kilombero na Mlimba,Kambangwa alisema kuna baadhi
ya wanachama walikihujumu chama na wao watakaa na kuwajadili kisha kuwachukulia
hatua.
Hata hivyo alisema kwa sasa uchaguzu umemalizika na watu wafanye
kazi na kuwata wananchi waondoe tofauti zao za itikadi na waijenge Kilombero
mpya na wao kama chama watahakikisha wanaisimamia serikali katika kuarakisha
maamuzi na kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji.

No comments:
Post a Comment