Wednesday, December 2, 2015

MAHAKAMA ya Kimbari ya Rwanda yafungwa

MAHAKAMA ya Kimataifa ya mauaji ya kimbari ya Rwanda (ICTR) iliyokuwa ikishughulikia kesi za mauaji yaliyotokea miaka 20 iliyopita imefungwa.

Mahakama hiyo iliyokuwa mjini Arusha Kaskazini mwa Tanzania ilikuwa ikisikiliza kesi za watuhumiwa wakuu wa mauaji hayo ya kimbari.
Sherehe za siku tatu zimefanyika kuadhimisha kufungwa kwa mahakama hii.
Waajiriwa wa sasa na wa zamani, mahakimu na mashahidi walikusanyika pamoja kuhudhuria sherehe hizo mjini Arusha
Baadhi ya matukio katika sherehe hizo yalikuwa ni pamoja na uzinduzi wa eneo la kubarizi al maarufu kama uwanja wa Amani, na kumbukumbu ya wahanga wa mauwaji ya kimbari


No comments:

Post a Comment