MKUU wa idara ya jinsia walimu wanawake CWT taifa
Mwandile Kiguhe akiwaasa walimu 17 waliostaafu ualimu Manispaa ya Morogoro.
|
CHAMA cha
walimu CWT manispaa ya Morogoro kimeendeleza mpango wake wa kumwaga vifaa
mbalimbali vikiwemo vya ujenzi na samani vyenye zaidi ya shilingi Mil.7,340,000
kwa walimu wastaafu sambamba na kuboresha mazigira ya kufundishia mashuleni.
Katika hafla fupi ofisi ya chama hicho mkoani humo,Katibu wa
Manispaa Raphael Munada alisema mbali na baraza la cwt taifa kupendekeza
walimum wasitaafu kupata bati kamati tendaji ya wilaya hiyo ilipendekeza mifuko
ya saruji ili walimu hao wakaboreshe makazi yao.
"baraza liliazimia kila mwalimu mwanachama apate bati zenye
thamani yashilingi 340,000 lakini kamati tendaji imepitisha walimu wetu
wastaafu 17 wapate mifuko 25 ya saruji kil mmoja yenye thamani ya shilingi
350,000...pia kuboresha maeneo ya kazi kwa kutoa samani vikiwemo viti vya
kisasa na plastiki"alifafanua Munada.
Mgerasimi mkuu wa idara ya jinsia walimu wanawake CWT taifa
Mwandile Kiguhe kwa niaba ya ya Makmu wa Rais wa chama hicho alisema mbali na
kuwa sehemu ya kuangana na walimu wanachama wastaafu ila imeboreshwa na kuwa
haki yao baada ya kuboreshwa katiba katika kifungu cha 6.2(d) toleo la sita
2014.
"niwaase! kustaafu sio mwanzo wa kuvunja na kukiuka haiba na
maadili ya utumishio wa ualimu,tunajua zipo changamoto nyingi zinawakabili
ikiwemo la mazoea ya utumishi lakini pia athari za kisikolojia na uchumi...kikubwa
mkaendelee kuwa mfano ulaiani"alifafanua Mwandile.
Aidha alisema kustaafu kwa utumishi sio mwisho wa kupta huduma
katika chama hicho ispokuwa huduma zitaendele kwao kwakua kwa mubu wa katiba
upo uananachama wa aina yingi ukiwemo wa ushiriki na ule wa kawaida.
No comments:
Post a Comment