Saturday, December 5, 2015

CHINA yaahidi kutoa dola bilioni 60 kwa nchi za Afrika

Rais  wa China Xi Jinping
RAIS wa China Xi Jinping amesema taifa lake litatoa ufadhili wa dola bilioni 60 kwa nchi za Afrika.

Tangazo hilo amelitoa kwenye mkutano mkuu wa ushirikiano kati ya Uchina na nchi za bara Afrika, ambao umeanza leo jijini Johannesburg. Viongozi kadha wa mataifa ya Afrika wanahudhuria.
Tangazo la fedha hizo za mabilioni ya dola ambazo zitatolewa kupitia ruzuku, mikopo na ufadhili wa miradi ya maendeleo lilisubiriwa, lakini kiasi cha fedha kilichoahidiwa kimezidi matarajio, mwandishi wa BBC aliyeko Afrika Kusini Karen Allen anasema.
Sehemu kubwa ya usaidizi huu wa kifedha sana utatolewa kupitia miradi ya miundo mbinu, kusaidia kusisimua ukuaji wa kiuchumi, lakini maelezo zaidi hayajatolewa.
Kiongozi mwenza wa mkutano huo Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesifu ushirikiano kati ya Uchina na nchi za Afrika.
Amesema watu wanaoishi Uchina na Afrika ni theluthi moja ya watu wote duniani, na kwamba hilo ni soko kubwa la bidhaa.
Uchina, nchi yenye uchumi wa pili kwa ukubwa duniani.





No comments:

Post a Comment