Mbunge
huyo Bw Justice Wadyajena anadaiwa kutumia “lugha ya matusi” dhidi ya
mwanachama mwenzake wa chama tawala cha Zanu-PF aliyekuwa ameweka picha ya Bi
Mugabe kwenye gari lake.
Kisa
hicho kinatazamwa na wengi kama sehemu ya vizozo ya ndani ya chama kuhusu nani
atamrithi Rais Robert Mugabe ambaye atatimiza umri wa miaka wa miaka 92
Februari.
Bw
Wadyajena amenukuliwa kwenye nyaraka za mahakama kwamba alimwambia Jimayi
Muduvuri: "Wewe ni mjinga sana, sawa na mama huyu wenu.” Atafikishwa
kortini Victoria Falls.
Mke
wa rais nchini Zimbabwe huitwa "amai", maana yake mama, na wafuasi wa
chama cha Zanu-PF.

No comments:
Post a Comment