Wednesday, October 26, 2016

DIWANI ashikiliwa na polisi kwa saa 30 bila ya kuelezwa kosa lake


Mkuu wa mkoa wa Morogoro Kebwe Steven Kebwe (Picha Michizi Blog)
DIWANI wa kata ya Kolelo wilayani Morogoro Erigius Mbena anadaiwa kushikiliwa na polisi kwa zaidi ya masaa 30 bila kuelezwa kosa kwa kinachodaiwa kuwa ni agizo la wilaya na mkoa.


Hata hivyo wilaya na mkoa kupitia wakuu wake akiwemo mkuu wa wilaya hiyo Regina Chonjo na Mkuu wa mkoa Dk Kebwe Steven wamekanusha madai hayo wakifafanua kuwa hata wao hawakuwa na taarifa hizo hadi walipoafiriwa na mbunge wa jimbo la Morogoro kusini mashariki Omari Mgumba.

“Nimerudi jana usiku kutoka Mahenge,usiku nikapigiwa simu na mbunge wa jimbo hilo bana Mgumba akinieleza taarifa hizo nikaagiza atolewe kwa dhamana na kama kunamambo mengine yamalizwe kupitia vikao na kama kunajinai basi polisi wafuate taratibu”alifafanua RC, Dk Kebwe.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya hiyo Regina Chonjo kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu ya kiganjani alikana kutambua taarifa hizo huku akimuuliza mwandishi nani kamwambia hivyo.

Mapema jana zilizagaa taarifa mjini Morogoro kuwa uongozi huo umeagiza kukamtwa mara moja Diwani huyo kwa kinachodaiwa kutumia vyombo vya habari kutangaza hali mbaya ya migogoro ya wakulima na wafugaji katani mwake.

Akizungumzia kukamtwa kwa diwani huyo Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Kibena Kingo aliliambia gazeti hili kuwa hali ya usalama kwa wanachi wilayani humo ni mbaya ikilinganishwa na inavyozungumzwa nje ya wilaya hiyo kwani baadhi wamekufa,kujeruhiwa na kutiwa vilema vya kudumu.

“ ngoja niongee kama diwani,ukweli hali ya kiusalama kwa wanachi wilayani kwetu ni mbaya ikilinganishwa na inavyoelezwa huko nje kutokana na ongezeko la wafugaji na hakuana hatua zichukuliwazo” alifafanua Kibena Kingo.

Kwa upande wake diwani Erigius Mbena alisema 21 Oktoba majiara ya asubuhi yeye na wenzie Venance Victory,Ezekil Adrian,Emili Adrian na Abdul Kiwanda kwa nyakati tofauti walikamatwa na mkuu wa kituo cha polisi Mvuha Afande Kanyika akisaidiwa na asikari wanne wenye silaha aina ya SMG.

No comments:

Post a Comment