Wednesday, October 26, 2016

MKUU wa wilaya ashiriki kuzima moto uliokuwa ukiteketeza milima ya Uluguru


Milima  ya Uluguru (Picha Shekidele Blog)

MKUU WA wilaya ya Morogoro Regina Chonjo mwishoni mwa wiki maeneo ya Kingolwira amelazimika kusitisha kwa masaa kadhaa msafara wake kutoka Morogoro - Mikese na kuanza kuzima moto uliokuwa umepamba moto kuteketeza mlima Urugulu.


Akizungumzia hali hiyo ambayo takribani wiki mbili sasa imeshuhudiwa milima ya Morogoro ukiwemo Urugulu,Mgulu wandege,Mindu na Lukobe ikiteketea moto na kuhatarisha uoto wake kuwa Jangwa Regina alisema tayari serikali imewaagiza viongozi wa seriakli za vijiji na Kata kuimarisha ulinzi dhiidi ya Moto.

“sina idadi wala majina kamili ya watu na viongozi wangapi wanaoshikiliwa na jeshi la polisi kuhusiana na tatizo hilo ili ila kunawatu wanashikiliwa na mieagiza wenyeviti wa vijiji na maafisa watendaji unakoaanzia moto kuwakamata wanao endeleza uharibifu huoo katika milima hii” alisema Regina.

Katika ufafanuzi wake Mkuu huyo alisema viongozi hao amewataka kuayatambua, kuwakamata waanzilishi wa moto kisha kuwafisha mahakamani bila kujali nia na makusudio yao.

“Endapo wahalifua hao hawatapatikana basi watakamatwa viongozi hao na kufungulia mashiataka mbalimbali likiwemo la kutotekeza amri ya mkuu huyo na kuwaficha wahalifu”

Alisema siku za karibuni karika mlima Urugulu,mindu,mzembe na mgulu wa ndege kumekuwa na moto ambao umekuwa ukitekeza uoto wa asili huku wanachi walio katika maeneo hayo hawachukui tahadhari kuukabili jambo linalohatarisha kutekeza uoto huo na kupoteza vyanzo vya maji na mvua.

Baadhi ya wanachi Stela Ramadhani na Pili Yahaya wa wakazi wa Kiroka waliozungumza na mwandishi wa gazeti hili  walisema kuibuka kwa moto huo katika milima hiyo unatokana na wanachi kuendeleza mifumo ya asili katika maandalizi ya mashamba bila kujali athari za ardhi, mimea mingine,wadudu na wanyama katika milima hiyo.

Katika miaka ya karibuni milima inayo zunguka mji wa Morogoro imekuwa ikiteketezwa kwa moto kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za mila na desturi,Kilimo,na uwindaji wa wadudu aina ya Ndezi na kudhibitiwa  kwa ushirikiano na serikali za vijiji,wanaharakati na taasisi mbalimbali za mazingira.





No comments:

Post a Comment