UDIKTETA wa
maamuzi Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro umeiingiza
halmashauri hiyo katika mgogoro mkubwa baina yake na wafanyabiashara wa soko la matunda na mbogamboga la Mawenzi likikusudia kwenda mahakamani.
halmashauri hiyo katika mgogoro mkubwa baina yake na wafanyabiashara wa soko la matunda na mbogamboga la Mawenzi likikusudia kwenda mahakamani.
Lengo la Kuifikisha
mahakamani linatokana na Halmashauri hiyo kuamua kubomoa choo kilichokuwa
kikitumika sokoni hapo awali na kuwalazimisha kutumia choo cha mwekezaji
anetoza shilingi 200 badala ya shilingi 100.
Mgogoro huo ambao tayari umezua vurugu na kusababisha Makamu mwenyekiti wa Soko hilo Hamprey Katabalula kuwekwa ndani kwa madai ya kuchochea vurugu, umeingia katika hatua nyingine ya wafanyabiashara sokoni hapo kwenda mahakamani.
Kwa nyakati tofauti baadhi ya wafanya biashara wakiungwa mkono na Mwenyekiti wa soko hilo Awadhi Mlonga walisema kwa muda mrefu manispaa imekuwa
ikiwarudisha nyuma katika maendeleo yao kwa maamuzi ya kidikteta.
"Mfano Mkurugenzi Jolvis Simbeye ameodoa viongozi wetu halali na kuweka wakwake wakati haipo kisheria, sasa ameweka uongozi wake anaoutaka na kutusababishia mgongano usio na tija kila kukicha"alisema mwenyekiti wa soko Mlonga.
Juhudi za mkurugenzi
wa halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Jolvis Simbeye kutoa ufafanuzi juu ya
sakata hilo hazikufanikiwa baada ya mkurugenzi huyo kumtaka mwandishi kupata
maelezo kwa afisa habari wa manispaa Lilian Heneriko ambae pia akataa kutoa
ufafanuzi huo kwa madai kuwa suala hilo ni kubwa na hana maelezo dhidi yake.Mgogoro huo ambao tayari umezua vurugu na kusababisha Makamu mwenyekiti wa Soko hilo Hamprey Katabalula kuwekwa ndani kwa madai ya kuchochea vurugu, umeingia katika hatua nyingine ya wafanyabiashara sokoni hapo kwenda mahakamani.
Kwa nyakati tofauti baadhi ya wafanya biashara wakiungwa mkono na Mwenyekiti wa soko hilo Awadhi Mlonga walisema kwa muda mrefu manispaa imekuwa
ikiwarudisha nyuma katika maendeleo yao kwa maamuzi ya kidikteta.
"Mfano Mkurugenzi Jolvis Simbeye ameodoa viongozi wetu halali na kuweka wakwake wakati haipo kisheria, sasa ameweka uongozi wake anaoutaka na kutusababishia mgongano usio na tija kila kukicha"alisema mwenyekiti wa soko Mlonga.
No comments:
Post a Comment