Makala

ULAJI UNAOFAA NA MTINDO BORA WA MAISHA 
Na mwandishi wetu
Makala hii inaelezea ulaji unaofa na mtindo bora wa maisha kwaajili yaafya na hali bora ya lishe ya mtu.Lengo la makala hii ni jinsi ya kuepuka magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza kama vile kisukari , magonjwa ya moyo, shinikizo kubwa la damu na aina mbalimbali za saratani kwa kuzingatia ulaji unaofaa na mtindo unaofaa.MAKALA hii inakujia kwa hisani ya Taasisi ya chakula na lishe Tanzania .Makala ina sura kumi na mbili fuatana nasi.

                                                       

                                                     SURA YA KWANZA
                                                   MSINGI WA LISHE BORA
Msingi walishe bora ni pamoja na kuzingatia ulaji unaofaa na mtindo bora wa maisha.Ulaji unaofaa ni ule unaozingatia milo mikuu mitatu ambayo ni kifungua kinywa, chakula cha mchana na chakula cha jioni/usiku.Milo hii inapaswa kuwa ya mchanganyikona yenye kiasi kilicho sahihi toka katika kila kundi la chakula na kwa  kila mlo.Kiasi cha chakula kutoka katika kila kundi kinategemea kiasi cha nishati unachopaswa kupata  kila siku.Kiasi hicho cha nishati hutegemea umri,jinsia , mazoezi na kazi mtu anazojishughulisha nazo.Mwili pia unaweza kuwa na mahitaji ya ziada ya virutubisho kwa mfano wakati wa ujauzito.
Mahitaji ya nishati kwa makundi tofauti ya watu
.Wanawake wasiojishughulisha na kufanya mazoezi na wazee wa jinsia zote wanahitaji nishati ya kadiri ambayo ni milo ianyoweza kutoa kilo kalori 1,600 kwa siku.
.Watoto , vijana wa kike , wanawake wanaojishughulisha na kazi za mikonona wanaume wasiojishughulisha na kufanya mazoezi wanahitaji kilo karoli 2,200 kwasiku.
.Vijana wa kiume,wanawake wenye kujishughulisha sana na kazi za mikono na wanaume wenye kujishughulisha nkwa kadiri wanahitajikilo karoli 2,800 kwa siku.
.Wanawake wajawazito wanahitaji kilo karoli 2,700 kwa siku.
.Wanawake wanaonyonyesha wanahitaji kilo karoli 3,000 kwa siku .
.Wanamichezo na wanofanya mazoezi ya kutumia nguvu mfano mpira, mieleka au riadha wanahitaji zaidi ya kilo karoli 3,000 kwa siku.
Inashauriwa katikakila molo kula kiasi sahihi cha chakula kutoka katika kila kundi .Kupima kiasi cha chakula kinachohitajika tunaweza  kutumia kikombe maalum(standard cup).
Vikombe hivi vinapima kiasi cha chakula cha ujazo wa ¼,1/2,3/4  na kikombe kizima.
Ili kurahisisha uelewa wa jamii vipimo hivi vimetafsriwa kwa kukadiria kiasi cha chakula mtu anachotumia kwa kutumia kiganja chake cha mkono.Ni muhimu katika kila kundi kiganja cha mkono kikatumika kupima kiasi cha  chakula kinachotakiwa.
 Makundi ya chakula yamegawanyika kama ifuatavyo
1.Vyakula vya asili ya  nafaka, mizizi na ndizi za kupika.
Vyakula katika kundi hili ni chanzo kikuu cha wanga.Vyakula hivi huupatia mwili nishati na joto .Unapaswa kutumia vipimo 6 hadi 11 toka katika kundi hili kulingana na uzito wako, umri wako, jinsia, n.k. Kwa wale wenye uzito uliozidi ni vipimo 6 hadi 8 .Vyakula vyawanga vimegawanyika katika sehemu kuu mbili.
   i)Vyakula ambavyo huyeyushwa kwa urahisi.
Vyakula hivi ni pamoja na nafaka zilizokobolewa kam vile mkate uliotengenezwa kwa unga mweupe, ugali wa sembe na mchelemweupe.Kwa kuwa vyakula hivi huyeyushwa na kufyonzwa kwa haraka, huongeza kwa haraka zaidi kiasi cha sukari mwilini.Ulaji wa vyakula hivi kupita kiasi huchangia ongezeko kubwa la uzito wa mwili hivyo kuwa na uwezekano wa kusababisha magonjwa sugu yasiyoyakuambukiza.
ii)Vyakula vya wanga visivyoweza kuyeyushwa na kumeng’enywa kwa urahisi  mwilini.
Kundi hili hujumuisha vyakula vitokanavyo na nafaka ambazo hazijakobolewa kam vile ugali wa dona, mtama, shayiri  na uwele.Vyakula vingine vilivyoko katika kundi hili ni pamoja na mchele wa rangi ya kahawia (Brown rice), vyakula vya asili ya mizizi kama vile viazi vikuu, ndizi na ming’oko.Vyakula hivi  vinamakapi kwa wingi , uyeyushwaji wake ni wa taratibu na hivyo kutoongeza sukari kwa haraka mwilini.Hali hii hupunguza uwezekano wa kupata ongezeko la uzito mwilini na hivyo kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa sugu.Uyeyushwaji wa vyakula hivi huchukua muda mrefu.
 Tumia kiasi cha ukubwa wa ngumi ya mkono wako kwa kupima kiasi cha mlo toka kundi hili, kipimo kimoja ni sawa na
     .Kipande kimoja cha mkate
     .Kikombe kimoja cha uji wa dona
     .Ngumi moja ya ndizi zilizopikwa
      .Nusu ngumi ya ugali wa sembe au wali mweupe
      .Chapati moja nyembamba
Katika kundi hili kikombe kimoja ni sawa na kadiri ya ukubwa wa ngumi yako.
Faida za vyakula vya asili ya nafaka, ndizi za kupikwa na mizizi.
 .Huupatia mwili nguvu na joto
.Vyakula vya wanga visivyoweza kuyeyushwa kwa haraka mwilini.
>Haviongezi kiwango cha lehemu mwilin
>Hupunguza uwezekano wa kupata saratani ya njia ya chakula
>Huzuia kuongezeka kwa uzito wa mwili kupita kiasi
>Huchelewesha ufyonzwaji wa sukari mwilini

2.Vyakula vya asili ya wanyama , jamii ya kunde na mbegu za mafuta:
Kundi hili lina  utomwili (protini)kwa wingi  na pia nishati, vitamini na madini .Utomwili ni muhimu kwa kujenga mwili, hutengeneza vimeng’enywa na kujenga upya sehemu za mwili zilizoharibika.Vyanzo vya utimwili ni pamoja na aina mbalimbali za vyakula vya asili ya wanyama, jamii ya kunde, mbegu za mafuta, na wadudu wanaoliwa.Unapaswa kutumia vipimo 2 hadi 3 kwa siku kwa chakula toka katika kila kundi hili.
 Tumia kiasi cha ukubwa wa kiganjacha mkono wako kwa  kupima kiasi cha mlo toka katika kundi hili.Kipimo kimoja ni sawa na ;
  .Kiganja kimoja cha karanga
  .1/2 kikombe cha maharage yaliyopikwa
  .Glasi ya maziwa yaliyoenguliwa mafuta
  .Kiganja kimoja kwa kila kipande cha nyam, kuku samaki.
Mambo muhimu ya kuzingatia
.Pendelea kutumia nyama nyupe mfano, samaki au kuku
.Tumia mara chache nyama nyekundu mfano ya ng’ombe au  nguruwe
.Toa ngozi ya kuku kabla ya kupika
.Toa mafuta yote yanayoonekana katika nyama kabla ya kupika
.Pendelea kununua nyama isiyonona
.Pendelea kuchoma, kubanika au kuchemsha nyama na si kukaanga.

3.Mbogamboga
Mbogamboga zina virutubishi aina ya vitamin na madini kwa wingi.Virutubishi hivi vinahitajika mwilini ili kuoboresha afya na kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya maradhi.Mbogamboga zinaweza kuliwa pasipo kipika , mfano kachumbari au baada ya kupika , mfano mchicha .Mbogamboga ni pamoja na mboga za majani , jamii ya mizizi mfano karoti, na mboga nyinginekam bamia , nyanya  na biringanya.
Unapaswa kutumia vipimo 3 hadi 5 kwa siku.
Tumia kiganja cha mkono wako kupima kiasi cha mbogamboga,kipimo kimoja ni sawa na
.Kiganja kimoja kwa mbogamboga zilizozopikwa
.Viganja viwili kwa mboga zisizopikwa (kachumbari)
.Supu ya mbogamboga nusu kikombe

Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kuandaa mbogamboga
.Zisianikwe au kuwekwa juani kwani ni joto la jua uharibifu vitamini.
.Zisioshwe kabla kukatwakatwa ili kuzuia upotevu wa vitamini.
.Zipikwe kwa muda mfupi kutegemea aina ya mbogana kiasi cha moto ili kuzuia upotevu wa virutubishi kama vile vitamini C.
.Zifunikwe wakati wa kupika ili kuzuia upotevu wa vitamin.
4.Matunda
Matunda huupatia mwili vitamini ambazo husaidia kuukinga mwili dhidi ya magonjwa na ufyonzwaji wa virutubishi vingine.Kwa mfano vitamini  C husaidia ufyonzwaji wa madini ya chuma.Kundi la matunda linajumuisha mapapai, maembe, manansi, matikiti maji, maparachichi, matufa na mapera.Mengine ni matunda pori ambayo ni pamoja na ukwaju,zambarau, ubuyu, furu, mabungo n.k.
Unapaswa  kutumia vipimo 2 au 4 kwa siku
Tumia ukubwa wa kiganja cha mkono wako kupima  kiasi cha matunda, kipimo kimoja ni sawa na
.Saizi ya kati ya chungwa, embe, ndizi n.k
.Saizi ya kati ya kipande cha papai, tikiti maji,nanasi n.k
.Juisi ya matunda glasi moja

Mambo ya kuzingatia
.Pendelea kula tunda kama lilivyo bdala ya kutengeneza juisi.
.Epuka kumenya tunda kama si lazima.

5.    Mafuta, Sukari na Asali
Mafuta, sukari na asali hutumika kam viungo , huongeza ladha ya chakulapia huupatia mwili nishati.Mafuta pia husaidia uyeyushwaji na ufyonzwaji wa vitamin A,D, E na  K.Mafuta ni pamoja nay ale yatokanayo na mimea kama vile karanga,alizeti na ufuta, mafutaya wanyama kama vile samli na siagi.Ikumbukwe kuwa mbegu za mafuta pia zina utomwili.Utumiaji wa vyakula hivi uwe kiasi kidogo tu.
Mambo ya kuzingatia.
.Usiache kutumia mafuta kabisa kwani yna umuhimu mwilini
.Pendelea mafuta yatokanayo na mimea, kuliko ya wanyama au yaliyogandishwa kama vile siagi
.Juisi ya matunda ina sukari ya asili hivyo haihitaji kuongezwa sukari
  
           KUMBUKA
.kula chakula mchanganyiko kwa afya bora
.Kula mboga mboga na matunda katika kila mlo
.Osha matunda kwa maji safi na salama kabla ya kula
.Zingatia usafi wakati wa kuandaa chakula
.Kipimo kiomoja ni sawa na ukubwa wa ngumi  au kiganja cha mkono wako.Ukiubwa wa kiganja chako unakupatia makisio ya kipimo cha kiasi unachopaswa kula






                                                      SURA YA PILI
VIASHIRIA VYA HATARI VYA MAGONJWA SUGU YASIYO YA KUAMBUKIZA
Viashiria vya hatari vya magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza ni vile vinavyoongeza uwezekano wa kupata magonjwa hayo.Viashria hivyo vimegawanyika katika sehemu mbili:vile visivyoweza kubadilika kabisa na vile vinavyoweza kubadilika kwa kurekebisha mtindo wa maisha .
Viashiria hatari visivyoweza kubadilika ni:
.Umri
.JInsia
.Viashiria vya kinasaba
Viashiria hatari vinavyoweza kubadilika pale mtindo wa maisha unaporekebishwa  ni pamokja na
.Ulaji usiofaa kama vle
   >Matumizi ya kiasi kikubwa cha vyakula vinavyotoa nishati (wanga, mafuta na utomwili)
  >Matumizi ya kiasi kikubwa  cha mafuta au vyakula vya mafuta
  >Kutokula au kula kiasi kidogo cha matunda  au mbogamboga
  >Matumizi ya vinywaji vilivyoongezwa sukari
  >Matumizi ya kiasi kikubwa cha chumvi
. Kutofanya mazoezi ya kutosha na kutojishughulisha na kazi za mikono.
.Unywaji pombe kupita kiasi
.Uvutaji wa sigara na matumizi ya tumbaku
Ulaji na mtindo wa maisha usiofaa kam ulivyoainishwa hapo juu,hupelekea mabadiliko kwenye mwili ambayo huwa viashiria vya hatari vya magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza.Viashiria hivi ni ;
.Uzito uliozidi na unene
.Ongezeko la lehemu mwilini
.Shinikizo kubwa la damu
.Ongezeko la sukari kwenye damu
Viashiria hivi huweza kudhibitiwa  kwa kubadili mtindo wa maisha

Ulaji na mtindo wa maisha usiofaa hujitokeza zaidi katika mazingira ya mjini.Watu wa mijini hupendelea zaidi kula vyakula vilivyokaangwa mfano chipsi mayai,vilivyotiwa sukari nyingi mfano kekina soda,vyakula vilivyowekwa chumvi nyingi mfano crisps na soseji.
Usafiri mjini unapatikana kwa urahisi hivyo watu hawatembei kwa miguu sana.Kwa wale wanaofanya kazi kwenye ofisi za magorofani hutumia lifti.Baadhi ya familia huajiri wahudumu wa nyumbani kusaidia kazi za mikono.Vyote hivi huchangia ongezeko la magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza mijini kuliko vijijini.





                             








                              SURA YA TATU
                              UZITO ULIOZIDI UNENE
Watu wengi hasa wale waishio maeneo ya mijini wana uzito au mafuta yaliyozidi mwilini.Unene ni hali ambayo mtu huwa na takribani asilimia 20zaidi ya uzito unaotakiwa kulingana na urefu wake .Hali hii inachangia uwezekano wa kupata magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza .Kuzidi kwa uzito kwa watu wazima hupimwa kwa kutumia Fahirisi ya uzito wa mwili (FUM) yaani Uwiano wa uzito katika kilogramu na urefu katika mita za mraba.Uwiano huu huitwa kwa lugha ya kingereza ni Body Mass Index(BMI)

FUM = UZITO(kg)
             Urefu(m)
M
fano mtu mzima mwenye uzito wa kilo 75 na urefu wa mita 1.7 FUM yake ni 75/(1.7*1.7)=75/2.28 =26 yaani kilogramu 26 kwa mita  moja ya mraba. 

   





              DENGUE FEVER                 DENGUE FEVER AWARENESS.
Dengue is a viral infection spread by mosquitoes.  It is widespread in tropical and sub-tropical regions. In the month of February 2014, the Dar es Salaam Public Health Officials confirmed a new wave of dengue fever cropped up in the most parts of Dar es Salaam and is still continuing.

The first ever recorded fever in Dar es Salaam was recorded in 2010 and in July last year. The Ministry reaffirmed that there were no confirmed death in either two past breakouts.(Tambwe M., Daily Newspaper, 8.2.2014)

Although dengue symptoms, when mild, can seem flulike, there is no vaccine or treatment for the infection other than staying hydrated and taking acetaminophen to manage the pain, other pain killers of the NSAID group like Ibuprofen & Diclofenac are not recommended as they can increase bleeding due to low platelet count (blood clotting cells). Those flulike symptoms also hamper public health officials’ ability to track the disease, because official surveillance of occurrences is based on medical reports and patients may not seek care for what they assume is a bout of flu. An estimated 50 million to 100 million dengue infections occur worldwide yearly, and severe forms of the disease can be fatal, especially among children. Beyond dengue’s death toll, its impact is largely felt in economic terms because sickened people cannot work or attend school.

Many people, especially children and teens, may experience no signs or symptoms during a mild case of dengue fever. When symptoms do occur, they usually begin four to 10 days after the person is bitten by an infected mosquito.

SYMPTOMS
The principal symptoms of dengue fever are listed below. Generally, younger children and those with their first dengue infection have a milder illness than older children and adults.
  • High Fever, up to 41ºC
  • Severe Headaches
  • Muscle, bone and joint pain
  • Pain behind your eye
Patient might also experience:
  • Widespread rash
  • Nausea and vomiting
  • Minor bleeding from your gums or nose
Most people recover within a week or so. In some cases, however, symptoms worsen and can become life-threatening. Blood vessels often become damaged and leaky, and the number of clot-forming cells in your bloodstream falls. This can cause:
  • Bleeding from the nose and mouth
  • Severe abdominal pain
  • Persistent vomiting
  • Bleeding under the skin, which may look like bruising
  • Problems with your lungs, liver and heart
  • Red spots or patches on the skin
  • Black, tarry stools (feces, excrement)
  • Drowsiness or irritability
  • Pale, cold, or clammy skin
  • Difficulty breathing
PREVENTION
There is no vaccine for preventing dengue.
The best preventive measure for residents living in areas infested with Ae. aegypti is to eliminate the places where the mosquito lays her eggs, primarily areas that hold standing water to stop mosquitoes from multiplying
  • Items that collect rainwater or to store water (for example, garbage cans, house gutters, buckets, pool covers, coolers, toys, flower pots, plastic containers, drums, buckets, any other containers, pet's water bowls, or used automobile tires) should be covered or properly discarded.
  • Protect boats and vehicles from rain with traps that don’t accumulate water.
  • Maintain swimming pools in good condition and appropriately chlorinated. Empty plastic swimming pools when not in use.
  • Clothing: Wear shoes, socks, and long pants and long-sleeves. This type of protection may be necessary for people who must work in areas where mosquitoes are present.
  • Apply mosquito repellent containing DEET
  • Use mosquito netting to protect children younger than 2 months old.
  • Cover doors and windows with screens to keep mosquitoes out of your house
  • Repair broken screening on windows, doors, porches, and patios.
  • Using air conditioning or window and door screens reduces the risk of mosquitoes coming indoors.
  • Proper application of mosquito repellents.
  • Mosquito Control: Use screens on doors and windows; use patio insecticides such as Permethrin (pesticide and repellent) and Allethrin (candles and lanterns. Wear long sleeve shirts, long pants, socks and closed shoes to avoid mosquito bites at dusk and dawn especial.
  • Use repellents containing DEET (N, N-diethyl-m-toluamide) or Picaridin on your clothing and exposed skin. Follow manufacturer’s instructions and CDC recommendations.
 TREATMENT
There is no specific medication for treatment of a dengue infection. Persons who think they have dengue should use pain relievers such as acetaminophen, other pain killers of the NSAID group like Ibuprofen & Diclofenac are not recommended as they can increase bleeding due to low platelet count (blood clotting cells). They should also;
  • Rest,
  • Drink plenty of fluids to prevent dehydration,
  • Avoid mosquito bites while febrile and
  • Consult a physician.
You should see your GP if you develop a fever or flu-like symptoms within two weeks of returning from an area where the dengue virus is common. If a clinical diagnosis is made early, a health care provider can effectively treat you. Kindly VISIT your nearest Health centre for advice and to test and confirm diagnosis of Dengue fever.






     ULAJI BORA KWA WATU WENYE UKIMWI
Kuishi na virusi vya ukimwi huathiri kinga ya mwili hali ambayo husababisha kuubgua marakwa mara na kupungua kwa uzito.Hali hii huchangia kuongezeka kwa mahitaji ya virutubishi mwilini ambavyo yasipokabiliwa  huweza kusababisha utapiamlo.Kuboresha hali ya lishekutasaidia kuimarisha kinga ya mwili na hivyo kupunguza makali ya UKIMWI.
Kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya virutubishi,mtu anayeishi na vvu anapaswa kuongeza kiwango cha vyakula vyenye  nishati,utomwili ,vitamin na madini.Virutubishi hivi vinazweza kupatikana kwa kula chakula mchanganyiko na cha kutosha kila siku.Inashauriwa kuwa na vyakula hivyo vitokane na makundi yafuatayo;
     .Vyakula vya nafaka,aina ya mizizi na ndizi za kupika
Kazi kubwa ya vyakula hivi ni kuupa mwili nguvu na joto.Vyakula katika kundi hili ni pamoja na nafaka kama vile mahindi,mchele ,mtama, ulezi,ngano,na uwele,aina ya mizizikama vile viazi,mihogo na magimbi na ndizi za kupika.
Nafaka zisizo zisizokobolewa zina virutubishi zaidi vya vitamini B na nyuzinyuzi  kuliko zile zilizokobolewa.Mara nyingi vyakula hivi huchukua sehemu kubwa ya mlo.Pamoja na na vyakula hivi kuupa mwili nguvu na joto ,vilevile huupa kiasi kidogo cha madini ,vitamini na utomwili.
      .Vyakula vya jamii ya mikunde,na vyenye asili ya wanyama    
Vyakula hivi huupatia  mwili utomwili kwa wingi ambao ni muhimu katika kujenga mwili na misuli.Vyakula vyenye asili ya mikundeni kama maharage,njegere,kunde,soya,njugumawe,dengu, na choroko;vyenye kokwa kama karanga na korosho.Vyakula vyenye asili ya wanyama ni pamoja na nyama,samaki,dagaa,maziwa,mayai,jibini,maini,figo,senene,nzige na kumbikumbi.Vilevile vyakula hivi huupatia mwili kiasi kidogo cha vitamin na madini.
      









.Mafuta na sukari
Mafuta na sukari huongeza nguvu na uzito wa mwili.Vyakula hivi pia huongeza ladha ya chakula.Vyanzo vya mafuta ni kama vile samli,siagi,ufuta,alizeti,kweme,mawese na karanga;na sukari hupatikana katika asali,miwa,sukariguru na ile ya kawaida.Asali  na sukari guru zina vitamin na madini kwa wingi kuliko sukari nyeupe.
     .Matunda
Matunda ni chanzo kizuri cha vitamini na madini.Virutubishi hivi husaidia kuimarisha kinga ya mwili.Kundi hili linajumuisha matunda kama vile mapapai,maembe,mapera,malimao,mapesheni,mananasi,peasi,ubuyu,ukwaju,machungwa na mabungo.
      .









Mbogamboga
Mbogamboga kama vile mchicha,majani ya kunde,matembele.mnafu,mchunga,majani ya maboga na karoti zina vitamini na madini kwa wingi.Vitamini na madini ni muhimu sana katika kuboresha kinga ya mwili hasa kwa watu wenye maambukizi ya VVU/UKIMWI.
Maji pia ni muhimu kuuwezesha  mwili kufanya kazi inayotakiwa.Inashauriwa kunywa maji safi na salama nay a kutosha kiasi kisichozidi lita 1.5ambazo ni karibu sawa na glasi nane kwa siku.Vinywaji vingine vinavyoweza kuupa mwili maji ni pamoja na madafu,togwa na maji ya matunda mbalimbali.
Vyakula vyenye nyuzinyuzi ni muhimu mwilini kwasababu humsaidia mtu aweze kupata haja kubwa kwa urahisi.Vyakula vitokanavyo na mimea kama vile mboga za majani,matunda,nafaka zisizokobelewa na jamii ya kunde zina nyuzinyuzi kwa wingi.Vyakula hivi ni kama viazi vilivyopikwa na kuliwa bila ya kumenywa,karoti,spinachi,kunde,mbaazi, maharage,machungwa na mahindi yasiyokobolewa.
 










Inashauriwa
.Kula chakula cha kutosha katika makundi yote ya vyakula kila siku
.Kuongeza kiasi cha matunda na mbogamboga
.Kutumia zaidi nafaka zisizokobolewa
.Kupika vyakula vya asili ya nyama mpajka viive vizuri.Vyakula hivi vikiwa havijaiva ni chanzo cha maambukizio
.Kuepuka unywaji wa pombe kwani hupunguza uwezo wa mwili kupata virutubishi muhimu
.Kuepuka uvutaji wa sigara kwani hupunguza hamu ya kula na kudhoofisha kinga ya mwili
.Kupunguza utumiaji wa vinywaji vyenye kafeine kwa wingi kama vile kahawa, chain a soda  na aina ya kola kwasababu huathiri ufyonzwaji wa badhi ya virutubishi
.Kuzingatia usafi wa mwili na mazingira ili kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya kuambukiza

3.0  Kukabiliana na matatizo ya kiafya yanayoambatana na VVU/UKIMWI kwa njia ya ulaji bora
  Kuna matatizo mbalimbali ya kiafya yanayoambatana na VVU/UKIMWI.Matatizo hayo yanaweza kuathiri mfumomzima wa ulaji,umengenywwaji wa chakula na ufyonzwaji wa virutubishi mwilini.Baadhi ya matatizo hayo yanaweza kukabiliwa kwa njia ya ulaji bora,nayo ni pamoja na  kuharisha,kukosa hamu ya kula na mabadilikoya ladha,vidonda na utando kinywani,kichefuchefu na kutapika.Matatizo mengine ni homa,kiungulia na vidondavya tumbo,kupungua uzito, upungufu wa damu,kukosa haja kubwa,kifua kikuu,kikohozi pamoja na matatizo ya ngozi.
3.1 Kuharisha
Inaendelea

.









 

              



 




2 comments:

  1. issa MSEKWA nitafurahi sana kama mtatimiza makala hii ya ulaji.nitaifuatilia mwanzo mwisho

    ReplyDelete
  2. Ulaji unaofaa ni somo zuri na tunahitaji makala nyingi zaidi ziwekanavyo ili tujifunze kuhusu namna ya kuboresha afya zetu

    ReplyDelete