Thursday, July 3, 2014

WADAU wa habari wampongeza Regina Mwoleka

 



Bi Regina Mwoleka kushoto akiwa na mtangazaji wa BBC

WADAU wa tasnia ya habari nchini wamempongeza mtangazaji nguli wa muda mrefu nchini Bi Regina Mwoleka kwa kuteuliwa kwake kujiunga na shirika la utangazaji la Uingereza BBC.
Wakiongea na mbiu ya Maendeleo  mapema jana , wadau hao wakiwemo waandishi wa habari wamesema kuwa, hiyo ni hatua ya maendeleo kwa B i Mwoleka na ni kielelezo kuwa wanawake wanaweza bila ya kuwezeshwa.
Regia Mwoleka ni mtangazaji wa kike wa muda mrefu ambpo alikuwa na Redio One na mpaka anateuliwa majuzi alikuwa akifanya kazi na kampuni ya Clouds Media Group

No comments:

Post a Comment