Maaskari wa JKT Ruvu wakilisha kuku |
TATIZO la upatikanaji wa nyama za kuku katika mikoa ya Pwani na
Dar es salaam limepatiwa ufumbuzi baada ya Jeshi la kujenga Taifa JKT Ruvu
mkoani pwani kuongeza kuzalishaji kutoka kuku wa kisasa 1200 hadi 3000 kwa
wiki.
Mbali na mafanikio hayo pia kambi
hiyo ya mafunzo ya awali ya kijeshi imefanikiwa kuongeza uzalishaji kuku wa
asili 270 hadi kufikia 1700 kwa wiki.
Hayo yalibainishwa mwishoni mwa wiki
na ofisa wa jeshi hilo Luthen kanali Charles Mbuge na kuongeza kuwa lengo
la kuongeza uzalishaji huo linatokana na kukua kwa soko la nyama za kuku badala
ya Ng'ombe na Mbuzi na kuliongezea pato na kukuza uchumi wa jeshi kupitia
uzalishaji huo.
"vijana mnajua ajira sio mbaka
uajiriwe na serikali au na mtu mkashinda mnapigizana kelele za kukatwa mishahara
na kutowajibika bali hata ukiamua kujiajili kupitia kilimo na ufugaji unatoaka
kimaisha"asema.
Nae daktari wa mifugo jeshini hapo
Jonathani Mgomi alibainisha changamoto wanayakabiriana nazo kuwa ni kuuziwa
madawa feki za mifugo kutokana na kukua kwa soko huria jambo linalorudisha
nyuma jitihada za jeshi kuondokana na umaskini.
Sanjali na hilo pia alisema ili
kuvutia soko tayari jeshi limepunguza bei za malighafi zinazo zalishwajeshini
kambini hapo kwa lengo la kuvutia wawekezaji katika sekta ya mifugo na kuwainua
wananchi wenye nia ya kufanya kazi hiyo ya ufugaji.
No comments:
Post a Comment