Monday, October 13, 2014

ASHIKILIWA na polisi kwa tuhuma za kukutwa na bunduki


Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro

JESHI la polisi Mkoani Morogoro linamshikiria Zahora Mwanang'ombe(42)Mkazi wa kijiji cha Luhembe kwa tuhuma za kukutwa na bunduki aina RYFOR 375 koking handle bila magazine ikiwa imefichwa ndani ya gunia la viazi vitamu.


Kamanda wa polisi Mkoani hapa Leonard Paul aliwaambia wanadishi wa habari mjini hapa kuwa tukio hillo lilitokea oktoba 12 majira ya saa 12 jioni huko Mikumi wilayani Kilosa.

Kwa mujibu wa Paul mtuhumiwa huyo akitokea Ulaya kuelekea Luhembe wilayani Kilosa
alikuwa akiisafirisha bunduki hiyo ndani ya viazi hivyo kwa njia ya Pikipiki Sanlg nyekundu isiyokuwa na namba za usajiri yenye chesesi namba LBRSTJB 5089037765.

Alisema kuwa mtuhumiwa huyo anashikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili mara baada ya kukamilika kwa uchunguzi.

WAKATI HUOHUO,MTU mmoja Latifa Abdallah(21)mkazi wa Kihonda Magorofani amejinyonga kwa kutumia mtandio ndani ya chumba chake.

Kamanda Paul alisema kuwa tukio hilo lilitokea oktoba 11 majira ya saa 5 asubuhi huko Kihonda Magorofani manispaa ya Morogoro.

Kamanda Paul alisema kuwa marehemu aliufunga mtandio huo juu ya kenchi katika chumBA alichokuwa akiishi huku chanzo cha tukio kikiwa bado hakijafahamika na uchunguzi zaidi ukiendelea.










No comments:

Post a Comment