Mkuu wa mkoa Morogoro Joel Bendera |
ZAIDI ya watu Mil.2.9 wenye
umri kuanzia miezi miezi sita hadi zaidi ya 100 mkoani Morogoro wanatarajiwa
kupata chanjo na kinga tiba ya magonjwa mbalimbali yakiwemo yasiyo pewa
kipaumbele katika tiba.
Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na mkuu wa mkoa Joel Bendera akiwaomba wanachi kushiriki kikamilifu katika kampeni shirikishi ya siku saba kuanza Oktoba 18 hadi 24 juu ya chanjo ya Surua rubella na kingatiba ya minyoo ya tumbo,usubi, matende na mabusha.
“wanachi watuelewe kuwa lengo la kampeni hii ni kukinga maambukizi ya Surua rubella,vitamini A kwa watoto,kinga na tiba kwa minyoo ya Tumbo,usubi, matende na Mabusha kwa watu wazima”alisema Bendera.
Katika ufafanuzi wake Bendera alisema takribani watoto 361,891 wenye umri wa Miezi 6 hadi miaka 5watapata chanjo ya Vitamini A,Surua rubella watoto 963,977 (miezi 9-miaka 15),Dawa za minyoo Mebendazole watu 316,286 (mwaka 1-5) wakati Dawa za minyoo,usubi,matende na mabusha Albendazole na Ivermectin wakikadiriwa kumeza watu 1,874,329(kuanzia Mika 5+)
Alisema ili kuharakisha zoezi hilo timu 507,watoa huduma 4000 wameandaliwa na watakuwa kwenye vituo vyote vya afya,ofisi zote za serikali na watu binafsi,taasisi zote yakiwemo mashule,vyuo na maeneo yote yenye mikusanyiko ya watu zikiwemo stendi,stesheni,masoko na vikao mbalimbali mitaani vitapitiwa na wahudumu.
“hapa niwaombe kwa dhati viongozi mashuleni, dini,sekta binafsi,wanasiasa wote kwa nafasi zao na viongozi wa serikali kuanzia mitaa kwa mjini na vitongoji kwa vijijini hadi wilaya hadi ofisi yangu kuelimisha wanachi juu ya umuhimu wa zoezi hili”aliongeza.
Katika hali isiyo ya kawaida mkuu huyo alikuta akikasirika ghafla na kufoka kuwa alichoulizwa si swali muda mfupi aliporuhusu maswali kwa waandishi nao kutaka kujua bajeti ya zoezi hilo mkoani humo.
“Hilo sio swali sisi tunazungumza mambo ya maana wewe unakuja na mambo yasiyo na tija…kama unataka kujua bajeti hii nenda wizarani au wasiliana na waziri mwenye dhamana”alisema kwa hasira na kuhitimisha kikao hicho ambacho mbali na wanahabari pia kilihudhuriwa na wataalamu kutoka idara mbalimbali za serikali mkoani humo.
Inakadiriwa zaidi ya watu mil40 kati ya zaidi mil 45 nchini wapo katika hatari ya kuambukizwa kuku watu mil.5 wakiwa waathirika wa magonjwa hayo.Mkoani Morogoro watu 920,000 wanakisiwa kuathirika na magonjwa hayo ambayo hudhibitika kwa njia mbalimbali ikiwemo umejai dawa(kinga-tiba).
No comments:
Post a Comment