Saturday, October 11, 2014

MASHABIKI wahukumiwa kifungo kwa kumtusi Rais Vladimir Putin


Mashabiki wakishangilia

MAHAKAMA  nchini Belarus, imewahukumu kifungo cha jela mashabiki wa soka kwa kuimba nyimbo za kumkejeli na kumtusi Rais wa Urusi Vladimir Putin.

Mwanamume mmoja alifungwa jela siku kumi kwa kuvalia nembo za kibaguzi. Wengine saba walifungwa jela kwa siku tano kwa kutumia lugha chafu.
Walikuwa wameungana na kuanza kuimba nyimbo za kumdharau Rais Putin katika mechi ya kufuzu kwa kombe la Euro mwaka 2016 kati ya Ukraine na Belarus.
Mashabiki kadhaa wa Bealrus pia walifungwa au kutozwa faini.
Mashabiki wote wa Belarus na Ukraine waliungana na kuimba wimbo ambao unasifika sana na ambao unaonyesha upinzani dhidi ya Rais Putin.



No comments:

Post a Comment