Tuesday, July 15, 2014

VYAKULA vyapatikana kwa urahisi soko kuu la Morogoro


Soko kuu la Morogoro 
UPATIKANAJI wa vyakula vya kutosha Mkoani Morogoro umewarahisisha waumini
wa dini ya kiislamu   kutimiza nguzo ya ibada kwa urahisi.



Upatikanaji huo umesababisha kushuka kwa bei za vyakula wanyama na ndege
watumikao kama kitoweo katika masoko yaliyopo mkoani hapa.

Uchunguzi wa uliofanywa na mwandishi wa habari hizi mwishoni mwa wiki
umebaini kushuka bei za vyakula kati ya shilingi 300 hadi 500 kwa rejareja
huku vitoweo vikishuka kwa kati ya shilingi 1,000 hadi 2,500.

Katika uchunguzi huo bei ya Mchela bora,maharage,jegere na unga wa sembe
imeshuka kutoka wastani wa Shilingi 2000 kwa kilo hadi 1500 wakati sukari
iliyokuwa inapatikana wa shilingi 2,000 sasa inapatikana kwa sh.1300.

Kushuka kwa bei hizo pia kumeiwezesha upatikana ji wa viazi
Mbatata,vitamu,mihogo na magimbi kushuka wastani wa fungu la shilingi 1000
hadi kufikia shilingi 500.

Aidha bei ya nyama buchani imeshuka kutoka shilingi 8,000 kwa kilo hadi
kufikia shilingi 4000 kwenye maduka ya nyama mjini Morogoro.

Hata hivyo baadhi ya wateja na wafanya biashara waliozungumza na mwandishi
wa habari hizi walisema upo uwezekano mkubwa wa bei hizo kushuka zaidi
kutokana na hali ya mavuno mwaka huu kuwa nzuri.

 Akizungumzia hali hiyo Katibu wa soko kuu Morogoro Chande Ramadhani
alisema mbali na kushuka kwa bidhaa hizo pia mapokezi ya mizigo kwa kipindi
hiki yameongezeka.

Aidha aliwataka wafanya biashara kuacha kupandisha bei ovyo kwa kisingizio
cha mahitaji kuongezeka kutokna na mfungo wa mwezi wa ramadhani

No comments:

Post a Comment