Monday, July 14, 2014

UNICEF yatahadharisha ya vita ya Gaza kwa watoto wadogo



 
Watoto waliouwawa shahidi na wanajeshi wa Israel

MFUKO wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (Unicef)  umetahadharisha kuhusu athari za kisaikolojia na kimwili za vita vya utawala wa Kizayuni kwa watoto wa Kipalestina wa Ukanda wa Ghaza.

Unicef imetangaza kuwa watoto wa Kipalestina wasiopungua 33 wameuliwa shahidi na mamia ya wengine kujeruhiwa katika mashambulizi ya hivi karibuni ya Israel huko Ghaza.
Taarifa ya Unicef imeongeza kuwa vita na machafuko vinaweza kuwa na taathira hasi kwa  mustakbali wa watoto na kwamba watoto wa Ukanda wa Ghaza wana matatizo mengi ya kisaikolojia na kimwili  yakiwemo na kuwa na jinamizi na msongo wa mawazo kutokana na kuendelea mashambulizi ya anga ya utawala wa Kizayuni katika eneo hilo.



No comments:

Post a Comment