Steven Mashishanga |
MKUU wa mkoa
wa Morogoro mstaafu Stephen Mashishanga amewaangukia viongozi wa dini nchini
akiwashauri kuacha kuwatia hofu ya uchaguzi waumini wao kwa kuhamisha ratiba za
ibada katika majengo yao ya ibada badala yake amewataka kujipanga
kwa hoja kuitaka serikali ijayo kuondoa siku za uchaguzi siku ya Jumapili.
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu nyumbani
kwake, Mashishanga alipendekeza kuwa na siku mbili za mapumziko maalumu kwa
ajili ya uchaguzi akiongeza siku hizo kuwa siku ya Jumatano na Alhamisi.
“ziwe siku za mapumziko kikatiba katika wiki ya mwisho ya mwezi
Oktoba na iwe siku ya Jumatano na Alhamisi kuepusha mwingiliano wa uhuru wa
imani…kumbuka kilakitu sasa hivi kipo kwenye mpangilio wa maisha sasa ikitokea
utaratibu ukabadilika unatengeneza tatizo lingine”alifafanua Mashishanga.
Alisema matamko ya viongozi wa dini likiwemo la ibada kufanyika
Jumamosi na kufanyika ibada moja badala ya utaratibu wa zamani unachochea
wananchi wenye hofu kukata tamaa ya kushiriki katika uchaguzi na matokeo yake
ni kupata viongozi wasio faa.
Kuhusu hali ya kisiasa kuelekea kwenye kampeni Mashishanga
aliyewahi kushika nyadhi mbalimbali tangu enzi za utawala wa awamu ya kwanza ya
Mwalimu Julius Nyerere, alisema uchguzi mwaka huu ni mzito na hautabiliki
kutokana na hamasa,shauku ya mabadiliko inayotajwa kuwepo.
Alisema kiongozi yeyote atakae chaguliwa katika uchaguzi huu anayo
haki ya kujidai na kujigamba kupata ushindi maana hali sio kama tuliyozoea hii
ni elimu tosha hata kwa utawala kutolegalega katika kuwatumikia wanachi.
No comments:
Post a Comment