Thursday, October 15, 2015

IDADI ya vifo vya mahujaji wa kitanzania vyaongezeka

IDADI ya raia wa Tanzania waliofariki katika mkanyagano wakiwa katika ibada ya Hajj nchini Saudi Arabia mwezi uliopita imeongezeka na kufikia 22,kulingana na waziri wa maswala ya kigeni.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari toka Saudia Arabia vinasma kuwa mahujaji wengine 38 kutoka Tanzania hawajulikani waliko.
Serikali ya Saudia imesema kuwa takriban watu 769 walifariki katika mkanyagano ,ijapokuwa maafisa kutoka mataifa wanayotoka mahujaji waliofariki wanasema kuwa idadi hiyo ni watu 1,480.
















No comments:

Post a Comment