![]() |
| Hospitali ya mkoa wa Morogoro |
HALI ya chumba cha kuhifadhia marehemu Hospitali ya rufaa mkoani
Morogoro ni mbaya.
Mbiu ya maendeleo Media imetembelea chumba hicho na kushuhudia miili
ya binadamu ikiwa imetapakaa sakafuni na kudondosha maji yenye harufu mbaya
hali inayotishia hata watumishi wa chumba hicho kushindwa kufanya kazi kwa
ustadi.
Baadhi ya ndugu,jamaa na marafiki wakisubiri kuchukua miili
ya jamaa zao wakizungumza kwa masikitiko kwa nyakati tofauti nje ya ya
eneo hilo,waliitupia lawama serikali kwa kushindwa kutenga bajeti ya kutosha
kuboresha na kuongeza majokofu yaliyokatika chumba hicho ili kichukue miili
mingi kwa muda mfupi.
“Hii siyo haki kwa nduguzetu kuwatelekeza chini na kuwacha
wakiharibika,ukweli hali hii ni mbaya kama unavyoona ukweli inatisha maana
marehemu wameachwa chini wanaharibika kama hawana jamii ya kuwasaidi kuwa
katika hali salama…serikali itafute uwezekano wa kuboresha hii ni nyumba
maalumu ambayo kila mtu ataipitia”alisema Mohamed Kipande wa Mwembesongo.
Walisema tatizo hilo limekuwa likijitokeza mara kwa mara kutokana
na serikali kupuuza kuongeza na kuyafanyia matengenezo ya mara kwa mara majokofu
yanyotumika kuhifadhia miili hiyo.
“tatizo la chumba hiki ni serikali kuto kijali kwa kukifanyia
matengenezo ya mara kwa mara ndio maana kinafanya kazi kwa kubahatisha,leo
ndugu zetu wana adhilika kama hawana ndugu tunaitaka serikali ilitatue tatizo
hili mapema na itenge fedha za ukarabati kila baada ya miezi mitatu…kumbuka
kunaongezeko kubwa la marehemu kutokana na ongezeko la watu mkoani hapa”alisema
Filimedia Kusaga.

No comments:
Post a Comment