Kiza Besigyakiwa chini ya ulinzi wa polisi |
MGOMBEA urais wa chama
cha upinzani cha FDC nchini Uganda Kizza Besigye amekamatwa na kuzuiliwa kwa
muda na maafisa wa polisi mjini Kampala.
Gari lake lilikuwa likipitia barabara ya Jinja, mjini Kampala,
msafara wake ukisindikizwa na mamia ya wafuasi, pale polisi walipotumia mabomu
ya machozi kuwatawanya wafuasi hao na wakamkamata mwanasiasa huyo.
Alizuiliwa kwa muda katika kituo cha polisi cha Kira Road lakini
akaachiliwa huru bila kufunguliwa mashtaka.
Polisi wanasema alikamatwa kwa sababu ya kutatiza
uchukuzi mjini.(Kwa hisani ya bbc
Swahili)
No comments:
Post a Comment