Wednesday, October 1, 2014

WANAWAKE Tunisia waendelea kupigania haki zao


Wanawake nchini Tunisia

WANAWAKE  nchini Tunisia wameendelea kupigania haki zao ili kushika nyadhifa za kisiasa kwa mjibu wa katiba ya nchi hiyo,hata hivyo baadhi ya wanawake wameanza kuonyesha wazi wazi jitihada za kujikomboa kiuongozi.

Katika hali ambayo haikuwepo siku za awali nchini humo kwa sasa baadhi ya wanawake wanahudhuria mafunzo ya wazi yanayowapa mbinu za kuwa wanasiasa wenye ushindani dhidi ya wanaume.
Kama ambavyo walionekana baadhi ya wanawake wakiwa wamekaa mbele ya mti huku wakiandika baadhi ya dondoo mhimu katika mafunzo yanayotolewa na taasisi moja isiyo ya kiserikali kuhusiana na mafunzo ya kisiasa kwa wanawake hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.


No comments:

Post a Comment