Saturday, June 14, 2014

CHUO cha kilimo Uyole chagundua aina tano za mbegu ya ngano





 
Rose Mongi mtafiti wa mbegu za ngano na maharage ARI-Uyole Mbeya


CHUO cha kilimo na utafiti Uyole mkoani Mbeya kimegundua aina Tano za mbegu ya Ngano zinazoweza kukabiliana na changamoto za kisayansi yakiwemo magonjwa,ukame na kuzalisha maradufu.


Mratibu wa zao la Ngano kutoka Wizara ya Kilimo,Chakula na Ushirika Antony Elanga alizitaja mbegu zilizogundulika na zinatarajiwa kusambazwa nchi nzima kwa uzalishaji kuwa ni SIFA, JUHUDI,LUMBESA,CHIRIKU na RIZIKI.

Hata hivyo alisema Uyole inakusudia kutatua tatizo la mbegu bora na zenye tija katika uzalishaji ili kufikia lengo la kulifanya taifa tegemeo kwa mazao ya chakula na yale ya Biashara hususani katika kipindi hiki cha uchumi duni
Mmoja wa wakulima Sevas Kabenga aliyewahi kupata nafasi ya kutembelea Ethiopia kujifunza kilimo cha Ngano alisema pamoja na ugunduzi huo wizara inastahili kueneza wagani na pembejeo kuwahishwa kwa wakulima.
 
Awali mchumi wa Taasisi hiyo ya kilomo Agnes Ndunguru na afisa Kilimo wa Halmashauri hiyo Maceline Mlelwa walisema zao hilo la Ngano ni la tatu nchini kwa kuhitajika licha ya uzalishaji wake kusuasua ikilinganishwa na mazao mengine ya chakula katika halmashauri Mbeya.


No comments:

Post a Comment