TATIZO
la uchafu wa mazingira katika masoko mengi jijini Dar es salaam uimeendelea
kuwa tatizo sugu ambapo hali ni mbaya zaidi na huenda wafanyabiashara na
wananchi wakakumbwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na kukithiri kwa uchafu.
Mbiu
ya Maendeleo ilitembelea soko la Ilala, jijini Dar es salaam na kuzungumza na
baadhi ya wafanyabiashara na wanunuzi wa bidhaa sokoni hapo, ambapo walisema
hakuna jitihada zozote zinazofanywa na mamlaka
za Halmashauri za wilaya na jiji jijini
Dar es salaam, kwani hali ni mbaya mno ilihali wafanyabiashara wanalipa ushuru
kila siku kwa manispaa na makampuni binafsi ya usafi lakini hali ni mbaya mno
kwa wafanyabiashara na afya ya walaji.
Hali
ya usafi wa mazingiara hasa katika masoko mbalimbali jijini Dar es salaam ni
tatizo sugu lililokosa ufumbuzi kwa muda mrefu sasa.
No comments:
Post a Comment