MFUKO
wa bima ya afya nchini NHIF
umekusudia kuondoa kero kwa wananchama wake hususani upatikanaji wa dawa kwa
wagonjwa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa
wa Bima ya Afya NHIF nchini Balozi Ali Mchumo,ameyasema hayo mapema leo mkoani
Tabora katika sherehe za mfuko huo zinazofanyika kitaifa nkoani humo huku
akiwataka wananchama wa mfuko huo kutokatishwa na tama na baadhi ya matendo
yanayofanywa na watendaji wa mfuko huo.
Wakati huohuo baadhi ya wananchi
mkoani Tabora wameutupia lawama uongozi wa juu wa mfuko huo kwa kuwanyanyapaa
baadhi ya wananchama ikiwemo kukaa madirishani kwa muda mrefu ambapo baadhi ya
wahudumu wa vituo vya afya, hospitali za wilaya,mikoa na rufaa kuonesha dalili
za kutojali wateja.
.
No comments:
Post a Comment