KESHO ni siku ya kuchangia damu salama duniani ambapo nchini Malawi
Taasisi ya kukusanya damu salama nchini humo imesema kuwa itafanya utafiti wa
kuchunguza kwanini wa Malawi wengi
hawachangii damu katika Taasisi.
Afisa mtendaji mkuu wa Taasisi
ya kukusanya damu nchini humo Bi Natasha Nsamala amesema, tafiti hizo
zitajikita zaidi katika kuchunguza sababu za watu wengi kutochangia damu.
Amesema kuwa,suala la kujitolea
damu halina malipo,lakini watu wengi nchini udai fedha kabla ya kutoa damu.
Amesema, asilimia 80 ya damu
zinazokusanywa nchini humo zinazotolewana vijana hasa wanafunzi wenye umri kati
ya miaka 16-25
No comments:
Post a Comment