Hopsitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro |
BAADA ya waandishi wa habari kuripoti hali mbaya chumba cha kuhifadhia
maiti Hospitali ya rufaa mkoani Morogoro,uongozi wa hospitali hiyo na mkoa
umekili kuwepo kwa hali hiyo nakuwaangukia wadau kupanua chumba hicho sambamba
na kununua majokofu.
Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Dk Riata Lyamuy a amewambia wandishi wa habari
mapema leo kuwa “hali hii imekuwa ikitokana na
uchache,uchakavu wa majokofu na udogo wa jengo hivyo kushindwa kukidhi mahitaji
ikumbukwe tumebakiwa na jokofu moja lenye uwezo wakuhifadhi maiti sita tu”
Dk.Rita alisema ingawa serikali imekuwa
inachukua hatua mbalilmbalimbali kuondoa kabisa tatizo hilo chumba hicho
kimekuwa tegemeo kubwa dhiidi ya marehemu toka hospitali,vituo vya afya na
zahanati zilizo Manspaa ya Morogoro na Halmashauri ya Morogoro.
“mbali na Miati hizo pia
kuna maiti zitokanazo na kuokotwa pia ajali zikisubiri kutambuliwa na
uchunguzi,vifo kutoka majumbani na matukio katika jamii”alifafanua Dk.Rita.
Alifafanua kuwa hadi
26/1/2016 waandishi wa habari wakiripoti
hali mbaya katika Mochwari hiyo,kulikuwa na maiti 12 zikiwemo tano zilizokuwa
zikisubiri kutambuliwa,tatu zilizotokana na ajali ya basi la kampuni ya
BM,maiti moja iliyotokana na ajali ya pikipiki na tatu kutoka hospitalini hapo
zikisubiri taratibu za mazishi.
Alisema tayari serikali
ikishirikiana na sekretarieti ya mkoa imetafuta wadau kusaidia kukarabati jengo
hilo sambamba na kuondoa majokofu chakavu yasiyotengenezeka kununua na kuweka
majokofu mapya ili kuongeza uwezo wa kumudu mahitaji.
No comments:
Post a Comment