Suakari ya magendo ikimwagwa |
MAKASHA 18 ya sukari yaliokamatwa katika
bandari ya Mombasa yakielekea Uganda yamefunguliwa na sukari hiyo kumwagwa baharini.
Mamlaka ya ushuru
nchini Kenya imesema kuwa bidhaa hiyo haikulipiwa na kwamba haikuwa bora kwa
afya ya binaadamu.
Kulingana na na
taarifa iliotiwa saini na kamishna wa mamlaka hiyo John Njiraini, Mamlaka hiyo
pia imekamata makasha mengine 63 yaliojaa mapipa ya Ethanol.
Mombasa
Njiraini amesema kuwa
vita dhidi ya biashara haramu vitaimarishwa kwa lengo la kuhakikisha kuwa wenye
biashara hizo wanashtakiwa.
No comments:
Post a Comment