Saturday, March 7, 2015

JAMII yakumbushwa kutunza na kuhifadhi misitu


Ukataji miti hovyo uhathiri maisha ya wanyama

WANANCHI  wilayani Kilosa,mkoa wa Morogoro wamekumbushwa kutunza na kuhifadhi misitu ya asili na ile ya kupanda ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.


Ushauri huo umetolewa jana  na Meneja wa wakala wa Misitu wilayani Kilosa, mkoa wa Morogoro, Bwana John Olomi wakati akiongea katika kipindi cha dira ya Mazingira kupitia redio  jamii ya Kilosa.

Amesema mabadiliko ya tabia nchi ni janga la kitaifa na kimataifa hivyo wananchi hawanabudi kushirikiana na wataalamu ili kukabiliana na hali hiyo. 

9 comments:

  1. Nasikia Kilosa kuna mkaa endelevu ,uko vipi huo?

    ReplyDelete
  2. Hongereni kwa kipindi cha mazingira, tunahitaji kuwahoji hao mabwana na bibi misitu, hasa kuhusu mkaa.

    ReplyDelete
  3. Nipo Dumila tupewe muda wa maswali.kipindi kinarudiwa lini?.Misitu ya hifadhi ni ipi?

    ReplyDelete
  4. Maaskari wa Misitu wanatuonea huku kijiji cha Mbwade, awatuhoji wala kutusikiliza.

    ReplyDelete
  5. Wataalamu wajena huku Parakuyo na Mkata.Hatuna elimu ya Mazingira na uhifadhi wa Misitu.John Haule

    ReplyDelete
  6. Wilaya na wataalamu wa mazingira wana mikakati gani ya kuboresha kilimo kilicho rafiki wa mazingira?Mbona wananvchi wanajilimia hovyo na kutumia mbolea bila kupta ushauri wa wataalamu?

    ReplyDelete
  7. Njooni kwetu mtembelee kijiji cha Ilonga, mtufundishe namna ya kuhifadhi na kutunza pia kulima miti.

    ReplyDelete
  8. Kipindi cha jumamosi iliyopita kilikuwa kizuri sana kuhusu tabia ya nchi.Kuna utaratibu gani wa kuwa elimisha watu wanaokata miti hovo ili kukabiliana na tatizo la tabia ya nchi?

    ReplyDelete
  9. Nilimsikia mtangazaji akisema wakala wa huduma za Misitu na neno TFS.Nini maana na kazi zao?

    ReplyDelete