Msitu wa Hifadhi |
Mhariri mkuu wa Mbiu ya
Maendeleo Media Group, Bi Salma Mlamila ameeleza kuwa kipindi cha
Dira ya Mazingira sasa kinarushwa hewani kupitia Redio Jamii ya
Kilosa, mkoani Morogoro.
Kipindi hicho kimeanza
kurushwa rasmi februari 16, mwaka huu katika kituo cha Radio Jamiii
kinachomilikiwa na Halmashauri ya wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro.
Kwa takribani miezi mitatu kipindi
hicho kitagusa sekta ya Misitu na kitakuwa kikizungumzia jitihada za wakala wa
Huduma za misitu nchini(TFS), hususani wilayani Kilosa katika
kutunza, kusimamia na kuhifadhi misitu .
Kipindi hicho kitakuwa kikirushwa
kila siku ya jumamosi saa tatu usiku.
Bi Salma Mlamila amewataka
wadau mbalimbali wa mazingira kukiunga mkono kipindi hicho kwa kushiriki
kipindi hicho, ambacho kitakuwa kikirushwa kila siku ya jumamosi saa tatu
usiku.
Amefafanua kuwa, makala
za vipindi hivyo zitakuwa zikipatikana katika blog ya Mbiu ya Maendeleo
ambayo ni www.mbiuyamaendeleo.blogspot.com
No comments:
Post a Comment